Kwa mujibu wa Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, Benghazi nchini Libya kila mwaka huandaa mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu yanayoshirikisha majaji mashuhuri wa kimataifa, mwaka huu, Libya itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo kwa mara ya kumi na tatu, ambapo zaidi ya washiriki 120 kutoka mataifa mbalimbali 75 watahudhuria.
Waandaaji wa mashindano haya wameeleza kwamba tukio hili la Qur’ani ni mujumuiko muhimu wa kuimarisha mshikamano na umoja miongoni mwa Waislamu, na pia ni jukwaa la kuwasilisha maadili ya Kiislamu, ambapo walimu na wahakiki kutoka Asia, Amerika, Ulaya na Afrika wanatarajiwa kushiriki.
Chanzo: LR
Maoni yako